Office Address

Ojijo Close, off Ojijo road next to Parklands Police Station

Phone Number

+254 740 047 047

Email Address

hello@tv47.co.ke

Sailors Gang wainama? Mmoja wao atangaza kujiunga na injili

Share
 • 14
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
  14
  Shares

Msanii Lexxy Young wa kikundi cha ‘Sailors Gang’ amejiondoa rasmi kutoka kikundi hicho na kujitosa katika muziki wa injili.

Young ambaye alishirikiana na wenzake kutoa vibao vikali kama vile ‘jeso ni mwathani’, na ‘wamlambez’ alifichua ari yake mpya kupitia akaunti yake ya Instagram.

 “Tumekuwa pamoja have done a lot and achieved what we set l wish you all the best in your journey, me nimeamua to take on gospel industry promise sitawainamisha uko and promise to always have your backs, gospel artists here I come,” Young alisema.

Maneno ya Young yamewaacha Wakenya wengi wakiwa katika hali ya ati ati wasijue kama ni ukweli ama ni kiki za kawaida za wasanii.

ALSO:  MORNING CAFE: The latest news stories making headlines in the country

Kwenye video hiyo, Young alimuomba msamaha meneja wao wa zamani Mwalimu Rachael na vile vile msanii ‘KRG the Don’. “My 10,000 reasons and my apologies @Mwalimurachel @Krgthedon.”

Wasanii wa kundi la ‘Sailors’ ambao walikuwa chini ya MRX Media Limited walitofautiana kimkataba na meneja wao wa zamani, ambaye pia ni mtangazaji Mwalimu Rachael mwezi wa Novemba mwaka wa 2020.

‘Sailors Gang’ baadae waliishia kufungua akaunti mpya ya YouTube baada ya Mwalimu Rachael kuwabania nywila za akaunti za awali (ukipenda “passwords”). Wakati huo, Mwalimu Rachael alidai kulipwa shilingi milioni 1.5 ili awape akaunti hizo za Instagram, Facebook na YouTube.

Hata hivyo mashabiki mitandaoni wanadai kuwa hii ni kiki, na kwamba kundi hilo liko jikoni kuandaa muziki utakaodondoshwa hivi karibuni.

ALSO:  "Our father was a fighter; but he was ready to go too"- Family eulogizes late MP

Hivi ni kweli msanii huyu wa Sailors amejiondoa ama tutarajie ngoma karibuni?