Office Address

Ojijo Close, off Ojijo road next to Parklands Police Station

Phone Number

+254 740 047 047

Email Address

hello@tv47.co.ke

OG, Nadia na Matata wateuliwa MTV MAMA Awards

Share
 • 6
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
  6
  Shares
In Summary
 • Msanii maarufu na ‘rapper’ kutokea Kenya Khaligraph Jones ameteuliwa katika kitengo cha ‘Best Hip Hop’.
 • Washindi wa tuzo hizi watatawazwa katika hafla inayotarajiwa kufanyika nchini Uganda tarehe 20 mwezi Februari.

Wasanii wa Kenya Nadia Mukami na kundi la Matata wameteuliwa katika tuzo za mwaka huu za  ‘MTV Africa Music Awards’ (MAMA) awards.

Wasanii wa Kenya Nadia Mukami na kundi la Matata wameteuliwa katika tuzo za mwaka huu za  ‘MTV Africa Music Awards’ (MAMA) awards.

Wasanii hawa waliteuliwa katika kitengo cha ‘Best Fan Base’, kitengo ambacho msanii mwenye mashabiki wa ukweli (Loyal fans) hutuzwa tuzo hilo.

Katika kitengo hicho, Nadia anashindana na wasanii mbali mbali wa Afrika ikiwemo; A- Reece na Cassper Nyovest wote wa Afrika Kusini, Diamond Platinumz wa nchi ya Tanzania, Eddy Kenzo wa Uganda, Fally Ipupa kutokea DRC, Naira Marley (Nigeria), Serge Beynaud (Ivory Coast) , Shatta Wale (Ghana) na mkali wa Nigeria Wizkid.

ALSO:  Shina la upeo: Latest news

Msanii maarufu na ‘rapper’ kutokea Kenya Khaligraph Jones ameteuliwa katika kitengo cha ‘Best Hip Hop’. The OG atashindana na magwiji kama vile Nasty C (Afrika kusini), 0MG (Senegal), NGA (Angola) Miongoni mwa wangine.

Kibao ambacho Papa Jones amemshirikisha Sarkodie, “Wavy”, kinafanya vizuri tu kwenye trends za YouTube nchini Kenya na Ghana. Tayari watu zaidi ya milioni moja wametazama video ya ngoma hiyo.

Katika kitengo cha ‘Artist of the Year’, watakaong’ang’ania ubabe ni Burna Boy (Nigeria), Master KG (Afrika Kusini), Davido (Nigeria), Wizkid (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria), Kalema (São Tomé and Príncipe), Diamond Platinumz almaarufu Simba (Tanzania).

Washindi wa tuzo hizi watatawazwa katika hafla inayotarajiwa kufanyika nchini Uganda tarehe 20 mwezi Februari.

Related Posts

Get Breaking News. Click Here...
Bulk SMS Kenya Breaking News