Office Address

Ojijo Close, off Ojijo road next to Parklands Police Station

Phone Number

+254 740 047 047

Email Address

hello@tv47.co.ke

Ilikuwa ‘cinemaree’, Eric Omondi afichua

Share
 • 28
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
  28
  Shares
In Summary
 • Wakenya wengi wamekuwa katika hali ya ati ati huku wasijue kama ni maigizo au ni ukweli Eric Omondi alikuwa anatafuta mke
 • Ezekiel Mutua alimshutumu Omondi kwa kueneza dhana potovu katika kipindi hicho.

Mcheshi Eric Omondi amefichua ukweli halisi wa kipindi chake cha “Wife material“.

Omondi amesema kuwa kipindi hicho hakikuwa cha ukweli bali kila kitu kilikuwa kimepangwa. Kumbe ilikuwa ni maigizo tu!

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya milioni tatu, Eric Omondi mwenye jina la utani “President of comedy in Africa – POCA” alisema, “Wife Material was a choreographed and Scripted Entertainment show.”

Wakenya wengi wamekuwa katika hali ya ati ati huku wasijue kama ni maigizo au ni ukweli Eric Omondi alikuwa anatafuta mke kama alivyokuwa akisema.

Kipindi hicho kilichoanza mwishoni mwa mwaka jana kiliwashirikisha watu mbalimbali ikiwemo akina dada wa kundi la muziki la “BAND BECCA’ (Caro na Becky), Shakila anayefahamika kama “Queen of Streets” miongoni mwa wasichana wengine.

ALSO:  Akothee's daughter Rue giving us the melanin magic

Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Nchini Ezekiel Mutua ni mmoja wa wale waliomshutumu Eric kwa kudai kuwa anaeneza dhana potovu ya kutowaheshimu kina dada.

“So there’s Corona but this fool has been kissing multiple girls and recording these videos in the name of comedy. Another morally bankrupt socialite is recording more videos teaching these young girls how to have sex with Omondi in the devilish mentorship program known as “Mombasa Raha,” Ezekiel Mutua alimaka.

Eric omondi ni mshindi wa tuzo mbali mbali, ya hivi karibuni ikiwa ni tuzo la ‘African Entertainment Awards USA’ (AEAUSA) za mwaka jana. Mkenya huyo aliibuka mcheshi bora Afrika.

Isitoshe, Omondi ndiye msanii wa kwanza ambaye yupo na wafuasi wengi nchini Kenya katika mtandao wa Instagram. Ana wafuasi milioni 3.1.

Related Posts

Get Breaking News. Click Here...
Bulk SMS Kenya Breaking News