Shakila Amuomba Wanyama Msamaha
Mwanasosholaiti Shakila amejitokeza wazi na kumuomba msamaha mwanasoka Victor Wanyama.
Kupitia kwa video aliyoipost kwenye page yake ya Instagram, Shakila alikiri kuwa hajawahi kukutana na kiungo huyo wa kati na wala hajashiriki uroda naye.
Shakila sasa anashikilia kuwa alikuwa mlevi chakari alipokuwa kweye ‘Instagram Live Chat’ na blogger X-tian Dela, na alisema maneno hayo kwa lengo la kutafuta kiki tu!
Isitoshe, kupitia live chat hiyo Shakila alikisia kuwa alikula uroda na wasanii wengi wa humu nchini, akiwataja Willy Paul na Khaligraph Jones kama baadhi yao. Itazingatiwa kuwa mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 19 pekee alimuomba msamaha Khaligraph Jones na kusema hawajatoka kimapenzi.
” I have never meet Victor Wanyama and I’m sorry for any pain I may have caused” alidokeza Shakila
Wanyama tayari ameshawasilisha kesi dhidi ya Shakila na X-tian Dela kwa kumharibia jina lake.

dhidi ya Shakila na Xtian Dela
Kwingineko ni kuwa Baada ya mfanyabiashara na fashionista tokea Zimbabwe Genius Ginimbi Kadungure kuaga dunia, majarida fulani yaliripoti kuwa Shakila aliwahi kupatana na Ginibi katika hoteli moja jijini Nairobi, ila shakila amejitokeza na kusema kuwa si ukweli na kuwa hamjui wala hawajahi patana na marehemu Ginibi
“I distance myself from this post I don’t know the late Ginimbi may his soul rest in peace . There are some things that are told online which are lies and my pictures are used”
Noti Flow aachana na mpenzi wake
Msanii wa Kenya Noti flow ameweka wazi kuachana rasmi na mpenzi wake kupitia mtandao wake wa instagram.
Msanii Noti Flow ametamba na vibao vingi ikiwemo “forehead” “100 barz” “ tupendane” aliyomshirikisha msanii Prezzo CMB na kibao kilichofanya vizuri mwaka huu cha “foto moto” alimchomshirikisha Alehandro Benzema kutoka kikundi cha ochungulo family.

Kupitia instagram stories zake, Noti Flow amesema kuwa “Mi si Size 8 ati you cheat on me then we blame the devil and pray for it..bruh……..”
Isitoshe kupitia comment moja, Noti Llow alimjibu shabiki kwa kusema “dump him before he dumps you in the future sis”.
Kabla ya kujitosa katika mahusiano na mpenzi huyu wa sasa, Noti Flow aliwahi kuwa katika mahusiano na msanii Colonel Mustapha, aliyetamba na kibao cha “lenga stress” mwaka wa 2009. Japokuwa hawajakuwa kwa muda mrefu na mpenzi wake toka alipomtambulisha mwaka huu, cha mno ni kuwa Noti hakuwahi kumtag katika post zake za Instagram na hivyo basi imekuwa vigumu kubaini jina la mpenzi wake.