Diamond anatafuta mpenzi mwingine?
Msanii na CEO wa lebo ya WCB Diamond Platinumz kutoka Tanzania kwa mara nyingine ameibuka na story ambazo wengi wametaja kuwa kiki za mjini, ila yeye bado hajazizungumzia. Wiki iliyopita msanii huyu aliyevuma na vibao kama “jeje na yope alipost picha ya msichana anayekwenda kwa jina Pat- Aika katika page yake ya instagram, kisha masaa machache baadaye aliweza kuitoa post ile. Cheche za bongo zinasema kuwa babake Pat- Aika ndiyo chanzo cha yeye kuondoa post hiyo katika mtandao wa insta.

Hamisa Mobetto alishika ujauzito wa Diamond mara tatu!
Mwanamuziki, mfannyabishara na fashionista Hammisa Mobetto aliweka wazi kwa kusema kuwa kabla ya kupata ujauzito wa Dylan ambaye ni mtoto wake Diamond Platinumz, alikuwa amepata ujauzito wa Diamond mara tatu huku ukiharibika. Kupitia mahojiano na kituo kimoja cha utangazaji Hamisa pia alisema kuwa hawajakuwa katika uhusiano mzuri na mama Dangote ambaye ni mamake mzazi wa Diamond, siku chache baadae mama Dangote alipost kupitia instagram yake akisema kuwa “ukoo haulazimishwi “

Zari anazicheki drama kwa mbaaaali!
Hayo yakijiri mzazi mwenza wa Diamond Zari Hassan, mzaliwa wa Uganda, ameonekana kuwa karibu sana na na mamake Diamond. Kupitia video ambazo mara kwa mara amekuwa akimrekodi mtoto wake Tiffah na kuzipost kwa mitandao, Mama Dangote amekuwa akizipost video hizo hizo kwenye Instagram page yake. Ukaribu huu wengi wameutafsiri kuwa kunao uwezekano mamake Diamond anajiribu kuficha zile tetesi kuwa yeye ndiye chanzo cha Diamond na Zari kukosana.
Kupitia caption ambayo Zari aliiweka kwenye insta yake alisema “vile tunazicheki drama kwa mbaaaali…” Ikichukuliwa kama anaangazia ugomvi kati ya Hamisa Mobetto na Mama Dangote.
